Juice Ya Ubuyu
LINK ::: https://urloso.com/2tDZPb
Ubuyu una kiwango kikubwa sana cha madini ya potasiamu. Kutokana na uwepo wa madini haya kunapelekea ubuyu kuwa na faida kubwa katika afya ya moyo kwasababu huusaidia moyo kwa kiasi kikubwa kusukuma damu.
Pia kuna madini haya ya kalshiamu na magnesiamu ambayo hupatikana kwa wingi katika ubuyu. Madini haya huusika kwa kiwango kikubwa katika uimarishaji wa mifupa. Madini haya ni muhimu hasa kwa wazee na watoto kwa kuwa mifupa yao kulingana na umri wao inahitaji madini haya kuimarika. Kwa watoto mifupa yao inahitaji madini haya kuweza kukua vizuri na kuzuia matatizo ya matege.
Kutokana na ubuyu kuwa na kiwango kikubwa cha madini ya chuma hupunguza hatari ya kupata magonjwa ya upungufu wa damu (Anemia). Kwasababu madini ya chuma huusika katika uzalishaji wa seli nyekundu za damu. Pia kwa mgonjwa wa upungufu wa damu mwilini kwa kutumia ubuyu kutamsaidia kuweza kurejesha kiwango chake cha damu mwilini.
Vitamin C hupatikana pia katika ubuyu. Vitamini C husaidia mwili kuzalisha seli nyeupe za damu kwa wingi. Seli hizi nyeupe za damu huusaidia mwili kuimarisha kinga yake dhidi ya magonjwa mbalimbali.
Mpaka sasa hakuna matatizo yoyote yaliyobainika kwa mtu kula ubuyu isipokuwa mafuta kutokana na mbegu za ubuyu yamebainika kuwa na kemikali ijuikanayo kwa jina la Cyclopropenoid fatty acids (CPFA). 781b155fdc